Mama anatakiwa apewe heshima zake zoooooote, analisha wanae wawili kwa pamoja na bado ana tabasamu zuri usoni kwake, huu ni upendo wa hali ya juu alionao
Mama anatakiwa asaidiwe pia kwenye majukumu mbali mbali na hili ni moja wapo
Mama huwa yuko tayari kuhakikisha familia yake inakula, hata kama ni kidogo wale kwanza watoto yeye baadae, kikiwa kingi ni furaha kwake kuwa familia yake itashiba vema na kupata afya
Mama anastahili apewe Busu takatifu kama hili ikiwa ni ishara ya kuonyesha upendo kwake na kuthamini ayafanyayo katika jamii
AKINA MAMA WOOOOOTE NAWATHAMINI SANA NA KUWAPENDA MNO, MUNGU NAOMBA UNIBARIKI NIWE MAMA BORA NA MWEMA NIWEZE KUITUNZA FAMILIA YANGU VEMA NA KUITHAMINI JAMII INAYONIZUNGUKA......AMEN