Sunday, July 22, 2012

LEO INATIMIA MIAKA MITATU TOKEA BIBI YETU MPENDWA MZAA BABA AFARIKI

Tarehe 22 mwezi wa 7 huwa ni tarehe ambayo twakumbuka siku ya kufariki bibi mzaa baba, kwa upande wa mama na baba huyu ndo bibi alikuwa kabakia na akawa ametufungia jalada la kuwa na bibi na babu. Huyu bibi alikuwa so close na mimi, shule ya msingi nimesoma nikiwa kwake na amenilea hasa...mama huwa ananiambia nilipofikisha mwaka mmoja alinipeleka kwa bibi huyu na nilikaa sana naye sikuwa msumbufu kabisa, wakati nimeanza secondary kila mwaka likizo moja nilikuwa lazima niende, hii ni picha nilipiga naye mwaka 2008 tulikuwa tumeenda kikazi sumbawanga nikapita kijijini kuwasalimia nikiwa na mama mdogo mtoto wake/mdogo wangu
 Hapa alikuwa anaumwa na tulipata nafasi ya kwenda kumuona ilikuwa miezi miwili kabla hajafariki
Padre alikuja kumtembelea pia na kupata sala
Na hapa ndo alipolala
Mwaka aliofariki mwaka huo huo mwezi wa 11 tulienda kijijini  familia zote kujenga makaburi ya bibi zetu wawili na babu zetu wawili upande wa mama na baba na tukafanya misa
Maakuli yalikuwepo
Mama na Vero
Mitambo kanisani ya wanakwaya
Wanakwaya wakiimba
Tulichagua nguo nyeupe kuwakumbuka akina bibi na babu, waumini kanisani
Nikiwa na baba shangazi/mumu wa shangazi yangu mwenye t-shirt nyeupe pia ni mwalimu wangu, na hao wengine ni wanafunzi wenzangu nilisoma nao darasa moja shule ya msingi
Mwenye nyeusi ni mwalimu wangu shule ya msingi, hadi leo huwa tunapigiana simu na kusalimiana, nikienda kijijini lazima nikamsalimie kwake
Kaburi la baba mzaa mama...yeye alifariki akiwa na miaka 106, nilikuwa darasa la sita ilikuwa ni siku ya ijumaa kuu...mama kwao ni mtoto wa mwisho
Kaburi la babu mzaa baba...alifariki nikiwa darasa la nne
RIP bibi.......am so connected na bibi huyu, ndo amenilea utoto wangu hadi darasa la 7, na alikuwa ananipenda mnoooo....i miss her mno
Wanachama wenzake wakitoa heshima zao kaburini kwake
Hapa yalikuwa ni maandalizi ya kujenga makaburi hayo manne
Ujenzi on process
Kaburi la bibi mzaa mama...yeye hatukwahi kumfahamu kabisaa maana alifariki wakati hata mama yetu hajaolewa
Kijijini hapo nilipata bonge la uyogaaaaaaaaa
Miaka yote hapa ndo twachota maji yanatoka milimani ni ya chem chem, tukitoa hapa ni kuyaweka mtungini yanakuwa ya baridiiii...hakuna kuchemsha wala nini
Idara nyeti
Ni hayo machache tu yaliyojiri miaka mitatu iliyopita
Upumzike kwa amani  Bibi Regina Namitita Matandiko.......Mungu alikupenda zaidi

5 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Ester pole nipo nawe katika machungu..najua ni jinsi gani. lakini kilichobaki ni kumwombea bibi yetu Regina. Bibi Regini ustarehe kwa amani.

Interestedtips said...

Asante sana dada Yasinta.....Amen

Anonymous said...

pole Ester. Mungu awafariji ndugu wote....pia nimependa picha ya uyoga mkubwa ulipendeza nao. Barikiwa

Unknown said...

Poleni sana dear kumbukumbu huwa zinaumiza sana...nimependa picha ya mwishooo umenikumbusha kijijini kupika kwenye kuni raha sana.

Interestedtips said...

Strictly and Majoy asanteni sana