Wednesday, April 25, 2012

TUKIWA TUNAELEKEA MEI MOSI – TOA HUDUMA BILA UPENDELEO



  1. Mtumishi wa Umma una haki ya kidemokrasia ya kuwa chama chochote cha siasa. Vile vile unayo haki ya kukipigia kura chama chako pamoja na viongozi wako wakati wa uchaguzi mkuu.
  1. Mtumishi wa Umma unaweza kushiriki katika masuala ya siasa katika chama chako ilimradi kwa kushiriki kwako hutaonyesha upendeleo katika utendaji wako wa kazi.
  1. Hata hivyo mtumishi wa Umma unapaswa kuzingatia masharti yaliyowekwa katika ushiriki wako katika masuala ya siasa:-
a)      Huruhusiwi kufanya wala kujihusisha na maswala ya siasa wakati wa saa za kazi au mahali pa kazi;
b)      Kutoa huduma kwa upendeleo kutokana na msimamo wako wa kisiasa; na

c)      Kutumia taarifa au nyaraka za kiofisi unazopata kutokana na utumishi wako kwa Umma kwa manufaa ya chama chako.

  1. Mtumishi wa Umma unayo haki ya kuwasiliana na viongozi au wawakilishi wako wa kisiasa ilimradi unazingatia yafuatayo:-
a)      Uepuke kutumia ushawishi wa kisiasa kuingilia mgogoro wa kikazi baina yako na serikali;

b)      Uepuke kutumia ushawishi wa kisiasa kwa manufaa yako binafsi ambayo sio sehemu ya sera za Serikali

  1. Mtumishi wa Umma unayo haki ya kuabudu na kushiriki dini yoyote unayoipenda ilimradi kwa kufanya hivyo huvunji sheria zilizopo. Hata hivyo, kwakuwa serikali haina dini, hairuhusiwi kuhubiri imani za dini wakati wa kazi na mahala pa kazi.


NI KATIKA KUKUMBUSHANA TU WAJIBU WETU MAKAZINI. NAWATAKIA KAZI NJEMA KWANI NDIO MSINGI WA MAENDELEO YETU NAWAPENDA WOTE, NA MSICHOKE KUTEMBELEA HUMU

No comments: