Friday, March 2, 2012

AKINA MAMA WAKIWA BUSY NA KAZI YA KOKOTO

 Maranyingi akina mama wengi huwa tuko busy kujishugulisha ili kuweza kutunza familia na kutatua mahitaji yetu
 Hili ni eneo la Tirdo upande wa nje wapo akina mama wengi wakivunja kokoto hapo na kuuza
 Waliniambia debe moja la kokoto wanauza 1500/-
 Mzigo uko tayari kuuzwa, wameshapakia kwenye mifuko
 Wananunua mawe, halafu wanatumia Nyundo kuyavunja vunja wapate kokoto
 
 Muda wa kupumzika hupatikana, hasa wakiwa wanasubiri wateja
 
 Wanavibanda vya kupumzikia pia
Pia wanapovunja mawe huwa zinapatikana chenga chenga za mawe nazo wanauza hasa kwa watu wanaokwenda kutengeneza tofali, wanasema tofali zinakuwa imara sana 
 Mifuko ya kujaza kokoto imerundikwa pembeni tayari kwa kuweka kokoto zilizo tayari
Hii picha ya huyu mama ni wa Sumbawanga vijijini, inaonekana hii kazi ni sehemu nyingi inafanywa na akina mama. 
Tukiwa tunaelekea siku ya wanawake Duniani, kujishughulisha na kazi za hapa na pale inasaidia kumuinua sana mwanamke, tufanye kazi kwa bidii ili tujikwamue na shida za hapa na pale, nawapenda Wanawake walio busy kujishughulisha, maisha ya siku hizi ni tata, kila kitu kimepanda bei

2 comments:

kokusimah said...

Jamani tuanyeje tuwaokoe kina mama Hawa? Wanahitadi ila wanatia huruma sana. Dada nilipiga hizo kokoto chuo cha ufundi Kama adhabu ya kuchelewa. Sina hamu nazo mie ntakutumia picha yangu nazo ahahaa utachekaje sasa nimetoka mbali jamani.

Interestedtips said...

Ni kweli wanatakiwa msaada, ila ni nani akawainue? i wish ningekuwa na uwezo huo ningefanya kitu, jikune uwezapo, nawahurumia sana, mimi nakumbuka kubeba Moram Nganza, lol