Mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya MyWay Entertainment, Paul
Maganga (Kulia) akielezea juu ya tamasha maalum la siku ya Wachaga lililodhaminiwa na Pepsi, litakalofanyika
siku ya Jumamosi Julai 28,Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni, ambapo pia
litasindikizwa na bendi za Msondo Ngoma, Twanga Pepeta na vikundi vingine vya
ngoma ya asili, (Kushoto) Ni Fredrick Mtaki, Afisamahusiano wa kampuni hiyo
BENDI zenye ushindani
mkubwa nchi za Twanga Pepeta na Msondo Ngoma zinatarajiwa kupiga shoo ya aina
yake kwenye tamasha la siku ya Wachaga, (Chagga Day 2012), Julai 28, viwanja
vya Leaders.
Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo ukumbi wa Udara habari Maelezo, ijini
Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Kampuni ya MyWay Entertainment, Paul Maganga walioandaa tamasha hilo
lililoadhaminiwa na kampuni ya SBC Tanzania Limited,kupitia kinywaji cha Pepsi,
alisema siku hiyo itakua ya aina yake
kwa watu mbalimbali na familia zao watakaojitokeza kufurahia kwa pamoja
tamaduni za kabila hilo la Wachaga sambamba na makabila mengine yatakayoshiriki
tamasha hilo.
“Siku hiyo ni ya pekee, kwa familia kujifunza mambo ya
utamaduni wa kabila hilo la Chaga, na
makabila mengine na burudani kutoka kwa
bendi hizo za Twanga na Msondo, pamoja
na vikundi vingine vya ngoma ya asili ” alisema Maganga
Pia alisema kua, kutakua na wazee wa mila ambo watazungumzia asili la kabila la
wachaga huku vyakula na vinywaji vya asili kutoka mkoa wa Kilimanjaro, Kiburu,
ndafu, shiro, kitawa, macharari, ngararimo, ng’ande, kisusio, mtori, Kisusio na
vingine vingi vitakuwepo siku hiyo.
Aidha, Siboka alisema
baada ya Tamasha la hilo la ‘Chaga day’, litafuatia tamasha lingine
litakalofanyika Mkoa wa Kilimanjaro, Desemba 22 ambalo litapambwa na sherehe
mbalimbali
Aidha, Maganga alisema kua, wataendelea kufanya matamasha
haya kwa karibu makabila yote yaliyopo hapa nchini ilikuwezesha jamii kutambua
mila zao sambamba na kudumisha utamaduni
wa Mtanzania kwa kuwakumbusha tamaduni
zao hii pia itakua ikijenga na kudumisha mahusiano baina ya makabila mbalimbali nchini Tanzania.
Pia anasema kua, watazania watakao hudhuria tamasha hilo,
watapata kujua chimbuko la kuweko kwa
tamaduni zao yaani mashujaa wa
makabila yao, viongozi na machifu waliotawala jamii zao.