Monday, April 9, 2012

STRESS FREE ZONE

Vyoo ni muhimu sana katika jamii zetu, kwani tunapotingwa hujikuta kuelekea hata porini ili tuweze kuchimba dawa. Lakini kwa maeneo ya makazi ni vema vyoo vikiwepo ili kujiepusha na maradhi/magonjwa ya milipuko. Hapo chini ni baadhi tu ya vyoo nilivyowahi kuvitumia katika zunguka zunguka yangu. Ni sehemu muhimu sana iafya, ila kila mtu ana namna aliyoipa kipaumbele kwenye ujengaji kiwe nadhifu au ili mradi paeleweke kuna choo.


1.
 Hiki kipo kijiji cha maeneo ya Bagamoyo
 Huu ni upande mwingine wa choo hicho cha juu


2.
 Huu ni ukuta wa choo kilichopo kijiji cha maeneo ya Bagamoyo


3.
 Hiki pia ni huko huko Bagamoyo, ukiingia choo cha wazi kama hiki, muda wote unajikoholesha ili mtu akitaka kuingia ajue kuna mtu
 Huu ni upande wa pili, sasa hapo ukiingia unaziba na kanga au taulo usionekane, ili upate nafasi ya kupunguza stress


4.
 Hiki niliwahi kukitumia Kigoma Vijijini
 Hapa ni sehemu ya bafu
 Pembeni ni Choo


5.
 Hiki kipo maeneo ya hoteli iliyopo Mahale Mountains - Kigoma, kimekaa kitalii zaidi
 Wamekitengeneza kwa kuvutia zaidi maana ni maeneo ya utalii


6.
 Hiki kipo Karema - Mpanda, hiki kipo wazi mno, nilishindwa kukitumia, maana nilishindwa nizibe wapi niache wapi


7.
 Stress free zone ya Beijeing


8.
 Hiki nilikitumia kijijini - Sumbawanga, kwa aliyemnene sana hiki hakitamfaa maana kilivyo inabidi upande juu, huwezi kukaa kwa usalama wa afya, 


9.
 Hiki nilikitumia Fryksas-Sweden, wenzetu nawapa credit kwa kujali hizi sehemu so smart


10.
 Stress free zone ya Clarion Hotel - Gavle, Sweden 

 Choo ni uhai, kipindu pindu kinaua, tujenge vyoo kwa afya zetu, kuna mahali pengine nimeenda unaomba sehemu ya kujisaidia unaambiwa hakuna choo, nendeni vichakani, tena ni kijijini, sasa kila mtu akienda kichakani, kijiji kitakuwaje? harufu ndo usiseme, magonjwa je?


NB: Samahani kwa yeyote ambaye nimemkwaza kwa picha hizi, kwani ndo afya zetu asilimia kubwa zina base hapa


Nawatakia mapumziko mema wadau wangu



No comments: