|
Kuna mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha St. Augustine Tabora alijinyonga last week, sababu haijafahamika bado, watu wakisambaa kutoka kushangaa tukio hilo, hatukuweza kupata matukio mengi ya picha ya tukio hili |
|
Ujenzi wa majengo ya Masters St. Augustine University Tabora |
|
Karibuni sana Tabora, siku hizi panapiga sana hatua, vyuo ndo kama hivi vinajengwa |
|
Majengo yanavutia hasa |
|
Kila jumamosi maeneo ya Ipuli karibu na kijiji cha Amani huwa kuna Mnada, hautofautiani na ule wa Dodoma |
|
Kwa wale wapenda nyama Choma mkifika Tabora siku ya Jumamosi utakutana na mambo haya mnadani |
|
Watu huwa ni wengi na boda boda za kutosha |
|
Biashara za nguo kama hivi ni kwa wingi |
|
Mifugo ndo mahala pake, unanunua, unachinjiwa unakula hadi meno yana feli kutafuna, lol |
|
Usafiri huu upo kwa sana, nikifikiria uzembe wao, kwa mimi nauogopa, wapenda kufika kwa haraka zana hizo hapo juu |
|
Matikiti sasa, matunda kwa afya zetu |
|
Vinywaji vya kusukumia nyama choma ili usinigwe, vipo tele |
|
Siyo Tanga tu, hata Tabora zipo nyingi, tena siyo za kisharobaro kama Tanga, hizi ni Phoenix mzee wa kazi, zinachanja Mbuga kweli kweli, ukikuta Msukuma anaendesha usipompisha fasta unaweza anguka mwenyewe hiyo speed halafu wana manguvu kweli, huku zatumika pia kama dala dala |
|
Uyoga jamani, na umiss sana, ukienda mnadani utaupata, hata kama ni kiangazi utapata ulio kaushwa |
|
Jamaa anasubiri haki yake, tuliagizwa tukavitawale, sasa tufanyaje? hata ndevu zikomae hadi ziote ukungu, lazima nyama ichomwe tushushie na kinywaji muruaaaaaaaaaaa |
|
Tabora pameshakuwa Nyumbani kabisaaaaaaaaa, msishangae napenda sana kuleta matukio yake, napenda mjue pakoje hasa kwa wale wasiopafahamu, siku hizi panapiga hatua sana, karibuni mjionee na mpate kujua watu wa huko wanaishije |
Na huyu ndo Reporter wetu wa matukio kutoka Tabora, Joseph Stima, asante sana kwa matukio haya
No comments:
Post a Comment