Unafahamu Ugalla River? Hizo ni baadhi ya picha zikiuonesha mto Ugalla
ambao umekuwa ukikauka siku hadi siku.zamani kulikuwa na imani kwamba
mto huo ni wa mizimu hivyo unaweza pita hapo mkamuona mwenye mto
akitokea katikati ya maji na kuomba
lifti ya treni na mkimyima basi treni haiondoki, hizo ni story za
zamani.…na kwamba kupita hapo bila kutoa sadaka basi mnaweza kukwama na
watu kwa imani hiyo wakawa wanatupia hela za kichele ili wavuke mto huo
salama..Imani hiyo ipo mpaka leo kwa baadhi ya
watu kwamba wakipita lazma watupie sadaka kwa mzimu wa mto huo lakini
cha kushangaza baadhi ya watoto wamekuwa wakisubiria pembeni ya daraja
la mto huo ili wewe unapotupia sadaka yako kwa mizimu basi wao
wanaokota......…HIZO NDO IMANI. TUBADILIKE,
Asante sana mdau wetu Veronica kwa maelezo hayo juu na matukio ya picha
No comments:
Post a Comment