Monday, April 16, 2012

RELI YA KATI TABORA - MPANDA

Naweza kusema nimekua nikiujua huu usafiri. Wakati wa kwenda likizo Sumbawanga ulikuwa ndo usafiri wetu, nilipokuwa naenda shule Mpanda Girls ndo nilikuwa natumia train, tokea miaka hiyo, nikijaribu kulinganisha wakati ule na sasa, kwa sasa huu usafiri una bore sanaaaaa, zamani ilkuwa raha mno, ikifika siku ya kusafiri mnafurahi, hizi picha ni za juzi, aliyetuma haya matukio alikuwa safarini ndo akayarusha, hata ratiba za usafiri zimevurugika mno, hazieleweki ndo maana watu wanatumia mabasi sana siku hizi, yaani shirika limeyumba mno, so sad
Hapa ni Mpanda Station, Enzi hizo maeneo ya kujidai wakati wa kufunga shule, mnashinda hapa hadi train ije ndo muondoke


Watu wakiwa busy na shughuli zao, wengine wakiwahi kupanda GOGO (Train)
Hapa ilikuwa ni sehemu tunanunua sana zawadi kama maharage, nyanya chungu, Lowe nk.
Tarin ikisimama biashara zinaendelea kama hivi Katumba Station

Hapa ni Tabora, mbele ya Jengo la Station

Na huyu Mfadafa Vero ndo aliyetuletea matukio yote haya, asante sana bi dada
Ki bongo bongo huwa tuna viita VICHWA VYA TRAIN, hizi ni Engine ndogo ziko 2
Hapa Tabora Station enzi hizo palikuwa panafurika sana wasafiri, palikuwa ndo kama centre ya reli ya kati, train kutoka Kigoma, Mwanza, Mpanda na Dar ndo zilikuwa zinakutana hapa, hivyo wizi ulikuwa ni mkubwa sana, watu walikuwa wanaibiwa sana, wasafiri walikuwa wanalala hapa, ilikuwa ni vululu vululu, kwa sasa pamedorora sana
Urambo station
Tabora station, unaweza sema mbona watu ni wengi, lakini miaka ile reli ya kati ilikuwa kwenye chart hawa watu ni kidogo, biashara zilikuwa juu hapa, vitabu vya hadithi za kila aina utakuta vinauzwa hapa, hadi vitabu vya shule
Baadhi ya mabehewa ya mizigo
Jamaa akifanya usafi Tabora Station
   
Serikali ina changamoto kuurudisha usafiri huu uwe kwenye chart kama zamani, siku hizi hata ratiba hazieleweki, kwa mimi zamani ulikuwa ukiniuliza kuhusu ratiba, nitakujibu ratiba zoooote, nilikuwa nazifahamu hasa, nilikuwa mdau mzuri sana, hadi muda wa kufika train iwe Dar, Tabora, Kigoma au Mpanda, nime umiss sana usafiri huu

No comments: