Thursday, April 26, 2012

HAPPY MUUNGANO DAY


WAPENZI NA WASOMAJI YA BLOG HII, NAPENDA KUWATAKIA SHEREHE NJEMA ZA SIKUKUU YA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR NA IKAZALIWA TANZANIA. LEO TUNATIMIZA MIAKA 48, TUTAFAKARI ZAIDI WAPI TUMETOKA NA WAPI TUNAELEKEA. TUFANYE KAZI KWA BIDII NA KWA USHIRIKIANO, MALUMBANO YASIYOFIKIA MUAFAKA HAYANA MSAADA KWA WATANZANIA, TUNACHOHITAJI NI KUSONGA MBELE KIUCHUMI, IKITAWALIWA NA AMANI TANZANIA BARA NA VISIWANI. TUKOMESHE WATUMIAO LASILIMALI ZA NCHI KWA MANUFAA YAO BINAFSI.
MUNGU IBARIKI TANZANIA
AMINA

4 comments:

John Mwaipopo said...

hata rangi za kivazi chako zimeungana vema.

Yasinta Ngonyani said...

Mungu ibariki Tanzania pia watu wake na dumisha amani na umoja pia uhuru..PAMOJA DAIMA:-)

Mija Shija Sayi said...

Halafu Ester wewe unajua una akili sana..!! Hiyo nguo yako nilipoiona tu nikasema Ester hatari, anatufikishia ujumbe kwa kutumia nguo yake pia. Gauni lako limeungana kutoka katika vitambaa vyenye rangi mbalimbali, rangi ambazo katika muungano wake zimetoa gauni moja safi sana. Hilo gauni litaendelea kupendeza kama hizo rangi hazitaanza kuchuja na kuingiliana, likitokea hilo basi gauni halitakuwa gauni tena bali mvurugano wa rangi.

Hii ni sawa sawa na Nchi yetu Tanzania..Tumeungana, tunapendeza katika muungano wetu na watu wengi sana wanatupenda sababu ya muungano huu. Kupendeza huku kunaweza kuendelea kupendeza iwapo tu, hatutaachia mianya ya kutokuchukuliana, kupendana na kulindana..

Asante Ester kwa Ujumbe wako, Mungu akubariki sana.

Heri ya Muungano.

Interestedtips said...

Da'Mija, Yasinta na John asanteni sana, twaombea Muungano wetu udumu zaidi, Da'Mija kagauni hako nimejitahidi kuweka material zisizochuja, naamini katadumu bila kuingiliana rangi, asante sana