Tuesday, March 27, 2012

HUDUMA BORA

Unapaswa ufahamu/utambue kwamba una wajibu wa kutoa huduma bora kwa umma. Katika kutimiza hilo kuna misingi ya kuzingatia:
1. Fahamu na kuheshimu kanuni za maadili ya kazi
2. Weka malengo halisi ya kazi ili kuwezesha kufikia kiwango cha juu kabisa katika utendaji wa kazi.
3. Kuwa mbunifu, mvumbuzi na siku zote kujibidisha kuongeza viwango vya utendaji kwa kujiongezea maarifa na ujuzi
4. Tumia misingi ya haki, badala ya upendeleo, katika utoaji wa huduma.
5. Uwe msafi na uvae nguo za heshima zinazokubalika mahali pa kazi.
6. Jitahidi kudumisha uhusiano mzuri mahala pa kazi na utendaji kazi wa pamoja kwa:
  • Toa maelezo ambayo ni wazi, sahihi na ya kueleweka;
  •  Epuka kufanya vitendo viovu au kutamka maneno yanayolenga kuwaaibisha watumishi wa ngazi moja, za chini yako au vyeo vya juu;
  • Epuka matumizi ya lugha mbaya, matusi, utani na hasira katika utendaji wa kazi;
  • Tafakari ipasavyo maoni rasmi yanayotolewa na wafanyakazi wengine na hata walio chini yako;
  • Fanyeni mikutano ya mara kwa mara na wafanyakazi;
  • Hakikisha kwamba wafanyakazi walio chini yako wanaweka malengo halisi ya kazi,fuatilia utendaji wao mara kwa mara na kuwahimiza kuongeza uwezo na ujuzi wao katika utendaji;
  • Toa taarifa za tathmini ya utendaji kwa wafanyakazi bila upendeleo;
  • Toa Sifa na Tuzo kwa wafanyakazi wenye utendaji bora na waadhibu wenye utendaji duni;

  • Waheshimu wafanyakazi wenzako na heshimu haki zao,hasa haki za faragha wanaposhughulikia taarifa zao za siri na binafsi.
NAWATAKIA UTENDAJI MWEMA WA KAZI POPOTE PALE ULIPO, HESHIMU KAZI YAKO KWANI NDIYO INAYOSABABISHA ULISUKUME GURUDUMU LA MAISHA, HESHIMU WATEJA WAKO MAANA NI WAO NDO HASA WANA PLAY PART KUBWA YA MALIPO NA MISHAHARA YETU, HUDUMA BORA NDO MPANGO MZIMA

MIMI PENDA NYIE SANA

3 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Ahsante kwa hili ni vizuri kukumbushana ukizingatia sisi ni binadamu..na hakuna aliyekamilika. Nakutakia utendaji mwema nawe pia...

Interestedtips said...

Asante sana dada Yasinta

kokusimah said...

Asante sis kwa kutustua, tunafundishana mamaa. Pamojaa