Pages

Sunday, April 13, 2014

REST IN PEACE MUHIDIN MAALIM GURUMO

Mwimbaji Mkongwe wa Bendi ya Msondo Ngoma Muhidin Maalim Gurumo amefariki alasiri hii katika hospitali ya Muhimbili alikokuwa amelazwa kwa matibabu baada ya kuugua kwa muda mrefu. Habari zilizofikia dawati letu zinasema kuwa mzee huyo amefariki kutokana na maradhi ambayo yalimsumbua kwa muda mrefu: 

Septemba 10, 2012: Mwimbaji huyo Mkongwe wa Bendi ya Msondo Ngoma alifanikiwa kupanda tena jukwaani kukonga mashabiki wa bendi hiyo baada ya afya yake kulega lega kutokana kusumbuliwa na Maradhi. 

Novemba 22, 2013: GWIJI wa muziki wa dansi mstaafu Muhidin Maalim Gurumo aliugua ghafla na kulazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es salaam. Mwimbaji huyo mkongwe alipatwa na tatizo la shinikizo la damu na hali ikawa mbaya kabla ya kukimbizwa hospitalini hapo.

No comments:

Post a Comment