JUMAPILI ILIYOPITA MJOMBA WANGU ALIKUWA KWENYE DALADALA AKITOKEA
UBUNGO KWENDA TEGETA.BASI LILIPOFIKA MWENGE ABIRIA WALIONGEZEKA NA WENGINE
WAKAWA WAMESIMAMA,KATI YA WALIOSIMAMA ALIKUWAPO MZEE MMOJA ALIYEKUWA NA HAND
BAG KAMA TUNAZOBEBEA LAPTOP HIVI, YULE MZEE ALIMUOMBA MJOMBA WANGU AMSAIDIE
KUMSHIKIA BAG LAKE KWA KUWA YEYE ALIKOSA SITI, BILA YA KUSITA AKAAMUA MUMSAIDIA
KALE KA BAG" BAADA YA VITUO VIWILI YULE JAMAA MWENYE KA BAG; ALITEREMKA
BILA MJOMBA WANGU KUMUONA NA YEYE HAKUWA NA WASIWASI KWA KUWA ALIJUA MWENYE
MZIGO AKITAKA KUSHUKA ATAUCHUKUA TU MZIGO WAKE.
KABLA GARI HAIJAFIKA KITUO CHA TATU ILISIMAMISHWA NA WATU
WALIOJITAMBULISHA KWAMBA WAO NI ASKARI POLISI WAPELELEZI KWAMBA KUNA KITU
WANAPELELEZA,WAKAWAAMURU ABIRIA WOTE WATEREMKE KWENYE GARI,WALIFANYA HIVYO
MMOJA WA WALE POLISI, WALIMFUATA MJOMBA WANGU NA KUMUULIZA 'NA WEWE KWENYE BAG
LAKO KUNA NINI? AKAWAJIBU BAGI SIYO LANGU KWA HIYO SIWEZI JUA NDANI KUNA NINI!!
WAKAMUULIZA TENA, MWENYEWE YUKO WAPI TUONESHE" AKAANGALIA KATI YA WALE
ABIRIA WENZAKE HAKUMUONA.
WAKASEMA FUNGUA TUONE KUNA NINI NDANI, WALIPOFUNGUA WAKAKUTA KUNA
SILAHA AINA YA PISTO.ALIPOJARIBU KUJITETEA WAKAMWAMBIA TWENDE KITUONI UTAENDA
KUJIELEZA HUKO. BASI LIKARUHUSIWA NA YEYE WAKAMPELEKA POLISI, WAKIWA NJIA
WAKAMWAMBIA KAMA ANATAKA WAMWACHIE ATOE LAKI NANE 800,000/= VINGINEVYO
WATAMUUNGANISHA KATIKA KESI YA WIZI WA KUTUMIA SILAHA,AKAWAAMBIA SINA HIZO PESA
NA SIWEZI KUTOA MPAKA SASA BADO YUPO NDANI.HII INATUKUMBUSHA KWAMBA NI KWELI
TUNAPENDA KUWASAIDIA WATU ILA TUWE MAKINI NA MISAADA TUNAYOITOA. MZEE ALIKUWA
NA NIA NJEMA KABISA YA KUTOA MSAADA ILA MSAADA UMEMGHARIMU MAISHA.
Mwisho
napenda kuwatahadharisha watu wote tuwe makini na watu tusiowajua,
jamani pole sana mjomba...Na Ester ahsante kwa taarifa hii. Ni kweli inabidi tuwe makini hata hii ya kumpa mtu usiyemjua lifti ni mbaya sana ...
ReplyDelete