Pages

Thursday, August 2, 2012

UPDATE YA MGOMO WA WANAFUNZI NA KUZIBA BARA BARA: KENYA

REPORTER WETU WA RURAL & URBAN BLOG ANASEMA: Kulikuwa tu na mgomo. WanafunzinHawakufurahishwa na kitendo cha mwalimu wao kuuza mbao za shule kwa wasomali kisha wakajenga msikiti shuleni kwao wakati kwa haraka haraka wengi wao inaonekana ni wakatoliki. Waliamua kuuchoma moto huo msikiti. Na tangu juzi usiku walikuwa wanapambana na maaskari waliotaka kuzima juhudi zao za kutangaza hoja yao. Ndipo asubuhi jana 1/8/2012 waliamua kufunga barabara eneo la KAJAIDO kama 100km toka Nairobi. Walizuia magari ya pande zote huku wakisema wanamtaka Waziri wa Elimu aje ili wamweleze. Sisi tulipofika tulikaa hapo kuungana na tuliowakuta kwa muda wa takribani masaa mawili. Mimi na Mmma mmoja na Mzee mmoja siwajui majina tulienda kuwaomba kuwa tunakwenda mbali waturuhusu tu tupite. Ila tukawashauri pia wajaribu kuongea mjumbe wa watu waliotumwa katika askari waliokuwa wamemwagwa wanasubiri amri tu. Tukawaambia mkishindwa wakaja polisi mtakosa hiyo fursa ya kuongea tena. Wakatusikiliza wakajikusanya wakajadiliana na kuanza mazungumzo. Na tukawaomba basi wafanyie mazungumzo pembeni ya barabara. Wakasita kidogo ila baadaye wakakubali. Ndio tukaendelea na safari.

Shukrani sana kwa Update hii

No comments:

Post a Comment