1 “Acheni kuhukumu ili msihukumiwe; 2 kwa maana kwa hukumu mnayohukumu, mtahukumiwa; na kwa kipimo mnachopimia, watawapimia ninyi. 3 Basi, kwa nini unautazama unyasi ulio katika jicho la ndugu yako, lakini hulifikirii boriti lililo katika jicho lako mwenyewe? 4 Au unawezaje kumwambia ndugu yako, ‘Niruhusu niutoe unyasi ulio katika jicho lako’; wakati, tazama! boriti limo katika jicho lako mwenyewe? 5 Mnafiki! Kwanza toa boriti lililo katika jicho lako mwenyewe, na ndipo utakapoona waziwazi jinsi ya kuutoa unyasi ulio katika jicho la ndugu yako.
6 “Msiwape mbwa kitu kitakatifu, wala msitupe lulu zenu mbele ya nguruwe, ili wasizikanyage-kanyage chini ya miguu yao na kugeuka na kuwararua ninyi.
7 “Endeleeni kuomba, nanyi mtapewa; endeleeni kutafuta, nanyi mtapata; endeleeni kupiga hodi, nanyi mtafunguliwa. 8 Kwa maana kila mtu anayeomba hupokea, na kila mtu anayetafuta hupata, na kila mtu anayepiga hodi atafunguliwa. 9 Kwa kweli, ni nani kati yenu ambaye mwana wake akimwomba mkate—je, atampa jiwe? 10 Au, labda, akiomba samaki—je, atampa nyoka? 11 Kwa hiyo, ikiwa ninyi, mjapokuwa waovu, mnajua jinsi ya kuwapa watoto wenu zawadi zilizo nzuri, je, Baba yenu aliye mbinguni hatawapa hata zaidi vitu vyema wale wanaomwomba?
12 “Kwa hiyo, mambo yote mnayotaka watu wawatendee ninyi, lazima mwatendee wao pia vivyo hivyo; hii, kwa kweli, ndiyo maana ya Sheria na Manabii.
13 “Ingieni kupitia lango jembamba; kwa sababu barabara inayoongoza kwenye uharibifu ni pana na kubwa, na wengi ndio wanaoipitia; 14 lakini lango ni jembamba na barabara inayoongoza kwenye uzima ina nafasi ndogo, na wachache ndio wanaoipata.
15 “Jihadharini na manabii wa uwongo ambao wanakuja kwenu katika mavazi ya kondoo, lakini ndani wao ni mbwa-mwitu wenye kunyafua. 16 Kwa matunda yao mtawatambua. Je, watu hukusanya zabibu kutoka kwenye miiba au tini kutoka kwenye michongoma? 17 Vivyo hivyo kila mti mzuri huzaa matunda mazuri, lakini kila mti uliooza huzaa matunda yasiyofaa; 18 mti mzuri hauwezi kuzaa matunda yasiyofaa, wala mti uliooza hauwezi kuzaa matunda mazuri. 19 Kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa ndani ya moto. 20 Basi, kwa kweli kwa matunda yao mtawatambua watu hao.
21 “Si kila mtu anayeniambia, ‘Bwana, Bwana,’ atakayeingia katika ufalme wa mbinguni, bali yule anayefanya mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni ndiye atakayeingia. 22 Wengi wataniambia siku hiyo, ‘Bwana, Bwana, hatukutoa unabii katika jina lako, na kufukuza roho waovu katika jina lako, na kufanya matendo mengi yenye nguvu katika jina lako?’ 23 Na hata hivyo nitawaambia waziwazi: Sikuwajua ninyi kamwe! Ondokeni kwangu, ninyi wenye matendo ya uasi-sheria.
24 “Kwa hiyo kila mtu anayesikia maneno yangu haya na kuyatenda atafananishwa na mtu mwenye busara, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba. 25 Na mvua ikanyesha na mafuriko yakaja na pepo zikavuma na kuipiga nyumba hiyo, lakini haikuporomoka, kwa maana msingi wake ulikuwa umejengwa juu ya mwamba. 26 Zaidi ya hayo, kila mtu anayesikia maneno yangu haya na hayatendi atafananishwa na mtu mpumbavu, aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga. 27 Na mvua ikanyesha na mafuriko yakaja na pepo zikavuma na kuigonga nyumba hiyo, nayo ikaporomoka, na anguko lake lilikuwa kubwa.”
28 Basi wakati Yesu alipomaliza kusema maneno hayo, umati ukashangazwa na njia yake ya kufundisha; 29 kwa maana alikuwa akiwafundisha kama mtu mwenye mamlaka, na si kama waandishi wao.
Mathayo 7:1-29
ReplyDelete1 “Acheni kuhukumu ili msihukumiwe; 2 kwa maana kwa hukumu mnayohukumu, mtahukumiwa; na kwa kipimo mnachopimia, watawapimia ninyi. 3 Basi, kwa nini unautazama unyasi ulio katika jicho la ndugu yako, lakini hulifikirii boriti lililo katika jicho lako mwenyewe? 4 Au unawezaje kumwambia ndugu yako, ‘Niruhusu niutoe unyasi ulio katika jicho lako’; wakati, tazama! boriti limo katika jicho lako mwenyewe? 5 Mnafiki! Kwanza toa boriti lililo katika jicho lako mwenyewe, na ndipo utakapoona waziwazi jinsi ya kuutoa unyasi ulio katika jicho la ndugu yako.
6 “Msiwape mbwa kitu kitakatifu, wala msitupe lulu zenu mbele ya nguruwe, ili wasizikanyage-kanyage chini ya miguu yao na kugeuka na kuwararua ninyi.
7 “Endeleeni kuomba, nanyi mtapewa; endeleeni kutafuta, nanyi mtapata; endeleeni kupiga hodi, nanyi mtafunguliwa. 8 Kwa maana kila mtu anayeomba hupokea, na kila mtu anayetafuta hupata, na kila mtu anayepiga hodi atafunguliwa. 9 Kwa kweli, ni nani kati yenu ambaye mwana wake akimwomba mkate—je, atampa jiwe? 10 Au, labda, akiomba samaki—je, atampa nyoka? 11 Kwa hiyo, ikiwa ninyi, mjapokuwa waovu, mnajua jinsi ya kuwapa watoto wenu zawadi zilizo nzuri, je, Baba yenu aliye mbinguni hatawapa hata zaidi vitu vyema wale wanaomwomba?
12 “Kwa hiyo, mambo yote mnayotaka watu wawatendee ninyi, lazima mwatendee wao pia vivyo hivyo; hii, kwa kweli, ndiyo maana ya Sheria na Manabii.
13 “Ingieni kupitia lango jembamba; kwa sababu barabara inayoongoza kwenye uharibifu ni pana na kubwa, na wengi ndio wanaoipitia; 14 lakini lango ni jembamba na barabara inayoongoza kwenye uzima ina nafasi ndogo, na wachache ndio wanaoipata.
15 “Jihadharini na manabii wa uwongo ambao wanakuja kwenu katika mavazi ya kondoo, lakini ndani wao ni mbwa-mwitu wenye kunyafua. 16 Kwa matunda yao mtawatambua. Je, watu hukusanya zabibu kutoka kwenye miiba au tini kutoka kwenye michongoma? 17 Vivyo hivyo kila mti mzuri huzaa matunda mazuri, lakini kila mti uliooza huzaa matunda yasiyofaa; 18 mti mzuri hauwezi kuzaa matunda yasiyofaa, wala mti uliooza hauwezi kuzaa matunda mazuri. 19 Kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa ndani ya moto. 20 Basi, kwa kweli kwa matunda yao mtawatambua watu hao.
21 “Si kila mtu anayeniambia, ‘Bwana, Bwana,’ atakayeingia katika ufalme wa mbinguni, bali yule anayefanya mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni ndiye atakayeingia. 22 Wengi wataniambia siku hiyo, ‘Bwana, Bwana, hatukutoa unabii katika jina lako, na kufukuza roho waovu katika jina lako, na kufanya matendo mengi yenye nguvu katika jina lako?’ 23 Na hata hivyo nitawaambia waziwazi: Sikuwajua ninyi kamwe! Ondokeni kwangu, ninyi wenye matendo ya uasi-sheria.
24 “Kwa hiyo kila mtu anayesikia maneno yangu haya na kuyatenda atafananishwa na mtu mwenye busara, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba. 25 Na mvua ikanyesha na mafuriko yakaja na pepo zikavuma na kuipiga nyumba hiyo, lakini haikuporomoka, kwa maana msingi wake ulikuwa umejengwa juu ya mwamba. 26 Zaidi ya hayo, kila mtu anayesikia maneno yangu haya na hayatendi atafananishwa na mtu mpumbavu, aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga. 27 Na mvua ikanyesha na mafuriko yakaja na pepo zikavuma na kuigonga nyumba hiyo, nayo ikaporomoka, na anguko lake lilikuwa kubwa.”
28 Basi wakati Yesu alipomaliza kusema maneno hayo, umati ukashangazwa na njia yake ya kufundisha; 29 kwa maana alikuwa akiwafundisha kama mtu mwenye mamlaka, na si kama waandishi wao.
Amen
ReplyDeleteAsante kwa kushirikiana nami katika usomaji wa biblia.Nathamini sana!!
ReplyDelete