Ilinyesha kidogo tu lakini ona maji yalivyojaa
Miundombinu ya barabara zingine kukosa mitaro ndo maana Dar asilimia kubwa huwa hatupendi mvua inyeshe
Ikinyesha hata robo saa, hiyo foleni yake ni balaa
Ona bara barani karibu na maeneo ya Salenda Bridge, mvua haikunyesha sana, lakini maji yalianza kujaa
Miundombinu hasa kuweka mitaro ya maji ni muhimu sana, sehemu husika iangalie hili, kwani inasaidia kuepusha mengi
Madimbwi kila mahali, pa kukanyaga tu ili utembee ni matope, sehemu kubwa maji yametuama
Du! jamani Tanzania yetu, maisha bora kwa kila mtanzania inasikitisha sana jamani. Mungu ibariki Tanzania na watu wake.
ReplyDelete