Pages

Tuesday, March 6, 2012

Kilimo kwanza - Langfang,China

Hizi ni plan zikionyesha makazi ya wakulima yaweje
Plan ikionyesha majengo ya huduma za jamii. Langfang-China, serikali ilifanya jukumu la kuwajengea wakulima makazi mazuri na yatakayomfanya mkulima awe katika hali njema na aweze kulima katika mazingira mazuri,rafiki yangu aliyeko huko Que Lief alinitext last week kuwa wakulima walishahamia wote kwenye nyumba zao, na kazi yao ya ukulima inaendelea kama kawaida, kipindi tupo kule ujenzi ulikuwa umepamba moto na ni baadhi tu ya wakulima walikuwa wamehamia kwenye nyumba zilizokuwa tayari

Hii Plan inaonyesha Community moja iweje, hadi garden zipo, hapo kuna kila hitaji la mkulima, kuna shule, hospitali, play grounds, masoko, nk. wamejitahidi kuweka kila hitaji kwa mkulima ili upate kila kitu hapo bila kuhangaika na kutafuta huduma nje ya Community
Baadhi ya mashamba
 Zinavutia
Baadhi ya wakulima na watoto wao
Tukisikiliza maelezo kutoka kwa wenyeji wetu
 Safi sana
Hizi ni nyumba za wakulima zikiwa tayari, na wanaishi humo kwa sasa, nilizitamani sana hizi nyumba,ndo zingekuwa TZ nadhani ambao wangeishi humo wangekuwa si wakulima, uchakachuaji ni mwingi sana nchini kwetu. je! Tanzania itafika lini stage hii ya kuwajengea wakulima makazi mazuri kwakuwa wanailisha nchi?

No comments:

Post a Comment