2. USIWAACHE WATOTO WADOGO WATEMBEE PEKE YAO BARABARANI.
3. USIWEKE VIZUIZI HOVYO BARABARANI PASIPO KUTOA TAHADHARI, USIWAZUIE WATUMIAJI WENGINE WA BARABARA KWA KUSIMAMA KATIKATI YA BARABARA YA WAENDA KWA MIGUU KWASABABU YOYOTE ILE.
4. USIFANYE MAANDAMANO AMBAYO HAYAONGOZWI NA ASKARI WA USALAMA BARABARANI AU HAYAZINGATII KANUNI NA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI.
5. USITUPE TAKATAKA HOVYO BARABARANI HASA VITU VYENYE NCHA KALI NA VITU VINAVYOWEZA KUSABABISHA UTELEZI NA HIVYO KULETA MADHARA KWA VYOMBO NA WATUMIAJI WA BARABARA.
6. USIMWAGE AINA YOYOTE YA MAFUTA BARABARANI, NI HATARI HUSABABISHA UTELEZI NA KUHARIBU BARABARA.
7. USIHARIBU ALAMA ZA BARABARANI.
8. USITEMBEE USIKU BILA TAA AU BILA KUVAA NGUO ZINAZONG'ARA ILI UWEZE KUONEKANA KWA URAHISI KWA WATUMIAJI WENGINE WA BARABARA HUSUSANI MADEREVA
ni kweli barabarani hakuna mchezo..tuwe makini
ReplyDeleteUjumbe mzuri, na ujumbe kama hizi zilitakiwa kuonyeshwa kwenye maruninga, ili watu, watoto wajifunze
ReplyDeleteDada Yasinta na Emu-three kweli kabisa, haya mambo hata waimbaji wasiyasahau kukumbusha watu
ReplyDelete