Pages

Thursday, October 18, 2012

PUSH MOBILE YAINGIA MKATABA NA KAJUNASON BLOG KUWAPA HABARI WANANCHI KWA NJIA YA SIMU ZA MKONONI KUPITIA SMS

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Push Mobile Limited, Bw. Freddie Manento akibadirishana mkataba na Mkurungenzi wa Kajunason Blog, Bw. Cathbert Angelo Kajuna mara baada ya Kajunason Blog kuingia mkataba na Push Mobile kuwawezesha wasomaji mtandao huu kupata habari kupitia simu zao za mkononi.
Ambapo mkurugenzi wa kampuni ya Push Mobile alisema kuwa wanafurahishwa na Kajunason Blog kuingia katika mfumo wa kuwapa habari wasomaji wake kwa njia ya Simu za Mkononi, "Kajunason Blog ni mtandao wa kwanza kuingia katika mfumo huu wa kurusha habari kupitia simu za mkononi," alisema.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kajunason Blog alitoa shukrani zake kwa kampuni hiyo na kuihakikishia kufanya kazi nao bega kwa bega ili kuweza kufikia malengo. Pia aliwaomba wasomaji kumuunga mkono kwa kujisajili ili wafaidike na huduma hiyo kwa kutuma neno KB kwenda 15678.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Push Mobile Limited, Bw. Freddie Manento akisaini mkataba wa makubaliano huku pembeni Mkurungenzi wa Kajunason Blog, Bw. Cathbert Angelo Kajuna akishuhudia. Mkataba huo umesaini ofisi za Push Mobile jiji Dar es Salaam.
Mkurungenzi wa Kajunason Blog, Bw. Cathbert Angelo Kajuna akisaini mkataba wa makubaliano na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Push Mobile Limited, Freddie Manento ambapo Kajunason Blog kuingia mkataba na Push Mobile kuwawezesha wasomaji mtandao huu kupata habari kutipia simu zao za mkononi.

No comments:

Post a Comment