Ukumbi ulipendeza hasa
Shughuli ni watu, kupendeza ndo ilikuwa mpango mzima
View ukiwa nje, dress code ilikuwa ni kiarabu
Msosi time, mambo ya Biriani,chapati,ndizi, mishikaki ya samaki,nyama nk.vingine nimesahu majina vilikuwa vitamu
Bibi harusi akiingia ukumbini, alipendeza hasa
Mikononi kachorwa hina matata, gauni nililipenda kwakweli
Hijabu za kila rangi, ukumbini ilikuwa ni harufu ya udi
Beautiful Ladies
Watu na camera zao busy na matukio
Sare zilikuwepo pia, Brown na Gold
Mume aliingia ukumbini baada ya Ndoa, vigeregere vikapigwa
Kila la Heri maharusi, Mungu awaongoze katika safari mliyoianza
Watoto hawakubaki nyuma, hadi wakasinzia
Wa kwanza kushoto mwenye Kiremba kichwani Faraji, ndo aliyetupa mualiko huu, shukrani sana
Photo session
Nadhani huyo mama pembeni ni somo wake, hakuwa mbali na bibi harusi
Walipendeza mno
Nilikosa nguo ya kiarabu nikatinga na ya Kihindi......chezea mnuso
Picha zingine asante Maggie tulikuwa naye hatukuweza hata kupata nafasi ya kupiga wote picha
Wamependeza kwa kweli nimependa mavazi yao maana wengi wanasema/fikiri ni nguo hasa gauni la bibi harusi ni lazima liwe jeupe.Mungu awape uvumilivu katika maisha ya ndoa. Ester nawe vituko eti nikatinga kihindi haya mdada umetoka chicha.
ReplyDeletealipendeza hasa mdada, yaani Yasinta nilitafuta kama nina hata Dera, holaa, nikutana na ya kihindi nikasema hii itanifaa, mbele ya Biriani duh
ReplyDelete