Ndo mshale unakuelekeza iliko
Sasa sijui ukifika hapa ndo uvae Ki Red Carpet kabisa kabla hujaingia eneo la tukio???
Sehemu wanayokusanya makopo ya maji na chupa za chai...unawauzia kwa kilo wananunua, wahi sasa kupeleka bidhaa zako, inasaidia sana kusafisha mji, siku hizi chupa za maji zilizotumika zimepungua sana mtaani
Wahi kabla hawajafunga...
Kiwanda kidogo cha kutengeneza koroboi
wakiwa busy na kazi
Penda na kuiheshimu kazi yako, ndo inayokupa heshima mjini au kijijini
Akaniuliza dada tukufungie mzigo wa kiasi gani??????
Nikamuuliza unauzaje kimoja? akasema kimoja 400/- ila ukinunua vingi tutakupunguzia bei
Nikaona si vibaya niwaungishe japo kimoja, soda na bia za kopo zikitupwa zinazaliwa bidhaa hizi
Nitawajuza nilimzawadia nani hiki kibatari...kopo la Redds limezaa kibatari, safi sana
Ukiona mafiga na sufuria juu ujue hatulali njaa siku hiyo
Team niliyokuwa nayo kazini mbagala, na mbwembwe zote za kunasa matukio mbali mbali kazi ilibidi ifanyike, hatukujali nyasi na vikwazo vingine
Watoto wakiwa wanaongozana hupenda kukimbizana ndo ilikuwa kwa hawa, huyo wa nyuma anachomoa mkanda wa suruali wakati mwingine upo begani akimwambia mwenzake subiri tubadlishane...
Sharobaro wa Mbagalaaaaaaaaa....style ya uvaaji wa kofia mi hoi
Kamandaaaaaaa
Hilo banda sio la kuuza hand bags, ila utaratibu ni kwamba mkifika job mnayaacha mabag yenu hapo, mnaenda kupiga kazi, mda wa kazi ukiisha unapitia hand bag yako unasepa home
Ahsante Ester! kwa kutotusahaou kuonyesha mazingira ya kunyumba nimejikuta kama tulikuwa pamoja...Kibatari kizuri... nimekipenda..Pia nimefurahi kusikia kuwa hakuna vyupa vya maji ovyoovyo maana duh!
ReplyDeleteEster unapakumbuka Makoroboi? Mwanza..
ReplyDeleteUmenikumbusha mbali sana mdogo wangu..
Da'Mija nikionaga tu koroboi, wazo la kwanza ni makoroboi Mwanza, yaani image ya kule huwa hainitoki
ReplyDeleteYasinta hayo mazingira ni ya Kunyumba kabisaaaaa