Pages

Monday, June 4, 2012

HII INAITWA FEATURING AU COLABOR

Tukaletewa full sinia limejaa wali wa nazi na samaki wale wadogo wadogo watamuuuu
Tukaanza Colabor yetu
Tukaendelea sinia linakuwa jeupe tuu
Hivi ndo msosi huwa unakuwa mtamu sana, ni juhudi zako tu ndo zitasema kama umeshiba au hujashiba
Ngwe ya kwanza ikaisha, sinia likawa tupu
Sinia likabebwa likajazwe part 2 iendelee
Featuring on process.........

Ukiona vijiko vinaanza kuwekwa chini kimoja baada ya kingine ujue matumbo yameshatosheka
Tukashiba...tukawa tunapumulia kwa juuu......hivyo ndivyo weekend yetu ilivyoisha, tulikuwa na mialiko mingi sehemu mbali mbali, huu ndo nilifanikiwa kupata tukio kwa kuwa lilinikumbusha style ya ulaji, sehemu nyingi hapa mijini hawali tena kwa style hiii, kila huyo anajipakulia kwenye sahani yake....mimi ulaji huu ndo nimekua nikiufahamu....na kijijini kwetu ndo mpaka leo ni hivi no mbwewe wakati wa kula no maongezi

JUMATATU NJEMA

4 comments:

  1. Ester sasa hapo mlikosea kweli yaani... kula na vijiko kweli?

    ReplyDelete
  2. hahahaha Yasinta ni ugenini nilishindwa kuwaambia tusitumie vijiko, kwani bila vijiko ndo ingenoga zaidi

    ReplyDelete
  3. Yaani si uwongo ingenoga mno..duh! masinia yote hayo:-)

    ReplyDelete
  4. mi pia huwa namiss sana ulaji huo...

    ReplyDelete