Pages

Wednesday, May 23, 2012

HADITHI HADITHIIIII............TRUE STORY ABOUT RURAL LIFE STYLE

Hapo kitambo kidogo.........tuliamka asubuhi ya alfajiri mida ya saa 11 asubuhi kujiandaa na safari, tulianza safari ilipofika saa 12 kamili asubuhi, tulikuwa twatokea Mishamo eneo la makazi ya wakimbizi lililopo Mpanda, kuelekea kijiji cha Bugwe-Mpanda.  Njia panda ya kwenda Bugwe kijijini ipo kati kati ya Makazi ya Mishamo na Mpanda mjini. Kutoka Mpanda mjini hadi Bugwe kijijini ni 76km. Kutoka Mpanda mjini hadi hiyo njia panda ni almost 40km. Na kutoka Mishamo hadi hiyo njiapanda sikumbuki ni km ngapi, ila tulitumia kama masaa mawili na nusu au matatu. Bara bara ni vumbi mtindo mmoja.......sasa tulipoingia njia ya kwenda Bugwe kijijini na kwakuwa tulikuwa hatupafahamu tulikuwa tunatumia ramani na kuuliza wenyeji ndo tukapewa uelekeo sahihi
Njia/bara bara hiyo sehemu zingine ni kama hivi miti imeshazama ikabidi tupite ingawa tilikwama kiduchu
Safari iliendelea bila kujali, njia si nzuri lakini tulichanja mbuga kukitafuta kijiji hicho
Kwakuwa maeneo mengi hakuna makazi ni pori, tulikuwa kimyaa garini kila huyo na mawazo yake, maana kutokea njia panda hadi tuendako ni kama 35km
Sehemu zingine ilitulazimu kupita maeneo ya mashamba ya mpunga, masika wanalima mpunga, waliotuelekeza walisema inabidi mmpite hapo hapo, ilikuwa kama tunacheza ngwasuma, gari linaruka ruka, hakuna kurudi nyuma, tukavuka eneo la mashamba
Maeneo mengine wananchi wametengeneza madaraja yao, kwani kipindi cha mavuno walisema magari yanafuata mazao sana, kwakuwa njia si nzuri inabidi walipie madaraja hayo
Na bei ni kama uonavyo wamebandika
Barabarani miti imeanguka sana, hatukuwa na jinsi, mnashuka mnasogeza mti au mnaukwepa, safari inaendelea
Na kwakuwa ilikua ni lazima tufike siku hiyo hiyo na kazi ifanyike siku hiyo hiyo halafu ni porini miti yote hii tuliikwepa safari ikaendelea
Madaraja kama haya ya wananchi njia hii yalikuwa mengi, tukajitahidi kuvuka na hili, Tukamshukuru mungu
Tulifanikiwa kufika kijijini hapo mida ya saa 7 mchana, tukafanya kazi iliyotupeleka na vifaa vyetu vikaanza kazi ya usomaji
Kwakuwa kutokana na uhalisia wa kazi ilikuwa inatulazimu kutoka hapo saa 1 jioni, na kwakuwa tuliamka alfajiri hatukuweza kupata hata chai, vijiji tulivyopita hawakuwa wanauza vyakula hivyo hatukuwa hata na akiba, vyote kwenye gari viliisha jana yake, ikabidi tuende kijijini tupate walau chakula, ndo tukamkuta bibi na wajukuuu kama hivi
Huyu mtoto alivunjika mkono, kwakuwa hakuna hata zahanati, wakamuwekea vimiti ili mkono usicheze wakamfunga na bandeji kwa juu, halafu akawa anakunywa asprini asubuhi na jioni, hii ilinigusa, mtoto alikuwa anapata maumivu sana, lakini hawakuwa na jinsi, wakiwa na dharura kali, mwenyekeiti anaenda mlimani anapiga simu ndo Ambulance inatoka mpanda mjini kwenda huko, imagine 76km na barabra ni mbovu, huyo mgonjwa atakutwa na hali gani???
Tukapata na photo session ya kijana huyu
Hii ni shule ya msingi ina walimu watatu tuuuu, tulipata nafasi ya kuzunguka na kuuliza mawili matatu, mazingira ni magumu sana
Hivi ni vibanda vya kuku
Issue kamili ilikuwa ni msosi, nashindwa hata kuelezea ilivyokuwa.....tulimweleza mwenyekiti wa kijiji tuna njaa, akasema hana akiba kabisa ya chakula, tukamwambia tutanunua kwa gharama yoyote, kwani hatujala tokea asubuhi hadi saa 8 mchana hii,ukweli alikosa hata kuku kijijini kote, tulizunguka holaaa, wanakiji wanajibu huu mwaka wa njaa na tulikuwa watatu tuuu, chakula kilikosekana, waka kaa viongozi kujadili tunafanyaje, wakamfuata baba fulani akawapa finyango 6 za nyama kavu, mke wa mwenyekiti ndo akatusongea ugali mkuubwa, ndo picha hiyo juu mwaiona, tukalumangia nyama kavu iliyokaushwa na ugali, tukashiba tukamshukuru Mungu. 

Tuliposhiba tukauliza ni nyama gani, hahahahahahha lol, tukaambiwa kama mmeshiba msiulize ni nini, nyie jalini mmeshiba, tukawa wapoleee.

Ilipofika saa 1, tukakusanya zana zetu za kazi tukaanza safari ya kwenda Mpanda mjini, tulifika saa 4 na nusu usiku, humo njiani no story tulikuwa twaomba tufike salama, tusipate hata pancha, hilo giza na ni porini mnashukaje mkipata adha, si unajua wanyama wakali na giza vinatisha. Tulipofika muda huo ni kutafuta sehemu ya kulala na tukapata,nakumbuka sikula usiku wa siku hyo ukweli nilichoka mnoooo.

NA HADITHI YANGU INAISHIA HAPA......Umejifunza nini kwenye hadithi hiii

4 comments:

  1. Haya ni mazingira ya kawaida sana kwenye nchii hii kama utakuwa unaenda sana sehemu za vijijini, mimi nimezoea kwa sababu tunazunguka na kuingia ndani sana wakati mwingine

    Ni muhimu kwenye gari kuwa na maji ya ziada kama lita 20, unga, dagaa, kisu, sufuria, tochi, vibiriti, kamba, shotgun na risasi za kutosha na vitu vingine vya safari za porini

    kwa kweli hali ya njia hizi ni mbaya sana na mshukuru mmeenda wakati wa kiangazi piga picha masika inakuwaje

    ReplyDelete
  2. Beneth usemalo ni sahihi, kwa wengine si kawaida na hawajawahi experience sehemu unazopita, huwa twafanya hivyo, kuna muda akiba inaisha kabisa kutoka na mnavyounga safari kutoka kijiji hiki hadi kingine, hahahaha kuwa na shortgun si hadi uwe na kibali maalumu, ila kuna maeneo hatarishi ndo police huwa wanatolewa mpewe escort ikitokea hatari mnasaidiwa

    ReplyDelete
  3. Ndo maana wanasema safari ni safari alosafiri kasafiri, My wii uwe unabeba vingi hasa matunda yakutosha, me huwa nkitoka utadhani sirudi siku hiyo. Imeniuma sana jamani. Mdogo wangu huyo namkono wake maskini anateseka tu, sijui kama anajua hata kama nchi yake ina uhuru miaka kibao na rais inaye. Ee Mungu atutazamie ndugu zetu nimeacha ku complain kwa kweli. Manake unatukuta kila saa sina hiki sina kile wakati wenzetu huko hawajui hili wala lile. Hadithi imenifundisha mengi hasa kuridhika na nilichonacho Kwani kuna wanaotamani
    Kuwa
    Nacho. Asante.

    ReplyDelete
  4. My wii uko sahihi, ila hadithi ni ndefu mnoo ningeweka yote ingeboa mkashindwa kuimaliza, ila huwa tuna beba vyakula, lakini for a month ni mnaamka alfajiri mnaenda vijijin msipopajua kufanya kazi kulala mbele kwa mbele, ndo mmerudi saa 5 usiku, asubuh alfajiri mnaamka kundelea na safari, hata mnakosa wapi mnunue vyakula vya kubeba, mkiwa mnafika mijini inakuwa angalau, ila kama mnaunganisha vijiji kwa vijiji hapo ni balaa, mnamaliza akiba, na kutokana na nature ya kazi, lazima mwende sambamba na wenzenu waliopo sehemu zingine ili upimaji uwe simultaneous na wa mikoa mingine.

    Huyo dogo wa mkono aisee, nilimuhurumia sana, labda alipona huko nyuma

    ReplyDelete