Tukikaribia siku za sikukuu maranyingi kariakoo huwa pako busy sana, na bidhaa nyingi huuzwa kwa mapunguzo ya bei, watu huwa wako busy sana na manunuzi, pata kuenjoy baadhi tu ya picha nilizopiga jana, ingawa ni nyingi ila ni baadhi ya zile nilizozinyaka. Enjoy
Lango kuu la kuingilia kariakoo ndani
Mitaa
Watu busy
Eti hii ni mitego ya panya, muuzaji alikuwa anasema ni ya kitechnology zaidi
Unapata viazi vikiwa vya motooo, inaivaa ikiwa kwenye torori inaiva
wachina hao, wakinunua maji kwa muuzaji
Kofia pia kwa wingi
Hili duka ni la wachina, wanauza wao wenyeweeeeeeeee, mapazia kibaoooo
Cashier ni dada mchina, nikamuomba anipunguzie bei akanijibu "HAILIPI" kiswahili kinapanda si mchezo
Huyu naye yupo duka hili, wapo wachina watatu, anasema tokea aje Tz ana mwaka mmoja, lakini kiswahili kinatamkwa hapo, duh
Nguo ndo usiseme
Wallet zimetandazwa chini kwa bei poa kabisa
Nunua mama upendeze kama uonekanavyo
Wale wa boarding school mwakumbuka Trancer?????
Ndo yamebaki mafungu sita awe amemaliza biashara
Wauza mifuko nao kazini
Urembo wetu wadada ndo huo
Pilau Pilau, viungo ndo hivyo vingi tu, siku ya pasaka ni pilau kwa kwenda mbele
Masufuria yanapendeza zaidi hasa ukisugulia hizi steel wool
Anauza Jiko
Hufi njaa ukiwa kariakoo
Hivi navyo vipo
Nawatakia maandalizi mema ya Pasaka
Mimi penda nyie sana
No comments:
Post a Comment