Pages

Wednesday, March 14, 2012

UHARIBIFU WA MAZINGIRA MTO MBEZI - DAR

Vijana wakibeba mchanga kutoka mtoni kupeleka juu yanapopaki magari ya kubeba
Vijana wapo busy si kidogo
Ona wanavyochota mchanga kwenye mto huo wanawauzia watu wa ma Lory
Hawajali kama ni uharibifu wa mazingira
Huo ni mto Mbezi, umejaa mchanga na watu ndo wamefanya ni sehemu ya kujichotea mchanga bila hofu
Mbali na kuharibu mazingira ya mto huo, kuna malipo yoyote yanafanyika serikalini au?
Au kuna vibali wanavyo bila sisi kujua?
Mimi nilipowauliza waliniambia kuwa wanaongea na wenye maeneo ili waweze kupata kwa kupark ma Fuso yao wapakie mchanga, na kuna hela kidogo wanawapa
Tuna mpango gani na mazingira haya?
Michanga toka mtoni imerundikwa tayari kupakiwa garini
Lory moja la Gari la mchanga wanauza shilingi 40,000/-
Biashara ndogo ndogo zikiendelea kando kando ya Mto Mbezi

No comments:

Post a Comment