Maranyingi nimekuwa na utaratibu hasa nipatapo nafasi kutembelea shule nilizosoma, Lengo ni kusalimia, kuona maendeleo na kujua Lipi linaloendelea kujiri shuleni hapo, hata ikibidi kutoa chochote nilichonacho hasa katika kuhamasisha wanafunzi wawe na moyo wa kusoma kwa bidii, Mwaka jana Nilienda kutembelea shule ya Secondary niliyosoma Form I hadi Form IV, na hii ilikuwa ni mara yangu ya 3 kwenda hapo katika nyakati/miaka tofauti tokea nimalize shule.
Jiko la Shule |
Wanafunzi wakisafisha mtaro wa maji machafu yatokayo jikoni |
Wanafunzi wakiwa busy kufua nguo zao, kwa nyuma ni Mabweni
Infirmary
School Assembly
TATA
Hili gari lipo hadi leo, na tulikuwa tunaambiwa lililetwa tokea shule ilipoanzishwa mwaka 1986 |
Nikielekea Duka la Shule kuongezea chochote kwa ajili ya wanafunzi
Baada ya maongezi na wanafunzi nikawagawia zawadi za mwanzo |
Unakumbuka mambo ya shule? "nitasoma PGM niwe Rubani, mara Nitasoma PCB niwe Daktari", hapa ni Main Switch, kwa tuliosoma nao watakuwa wanakumbuka,niliwahi kupewa jukumu la kuzima na kuwasha umeme chumba hiki, Kila ikifika saa 1 kamili jioni naenda kuwasha umeme, na ikifika saa 4 kamili usiku naenda kuzima, shule inakuwa giza hasa, kwani umeme ni wa Genereta na sio Tanesco, nilipita kupaona, kujikumbusha zaidi,kwani hii kazi ilinipelekea kupenda kusoma mambo ya Umeme, hadi ilinibidi nisome PCM, leo hii nipo fani tofauti na umeme, ndoto hizi jamani
Story za hapa na pale na walimu na wanafunzi
Nilipelekwa pia Maabara, siku hizi hii shule kuna Form V na VI, wakati twasoma siye ilikuwa ni O'Level tu |
Wanafunzi wakinionyesha mambo ya maabara, nilipokelewa vizuri sana hadi raha |
Dereva Sanga wa TATA, aliponiona alifurahi sana, amekuwa akiniona mara kadhaa, hajanisahau, akituchekesha hapo, ni dereva wa kitambo sana, na bado yupo hapo shule |
Nikiwa Staff Room na mwalim
Msomaji wangu, mara ya mwisho ulitembelea lini shule uliyosoma? hata kama ulikuwa mtukutu vipi, unachapwa sana, wewe kipanga sana, hata shule ya msingi tu, ipo siku nitapost nilipoenda shule yangu ya msingi kubarizi na kuperuzi kijijini kwetu, mi naona ni jambo jema mno, linasababisha tukumbuke mambo mengi, pia wanafunzi wakifahamu ulisoma pale wanajua kuna ku-move forward, mwenye experience hiyo naomba atutumie kupitia ester.ulaya@gmail.com, ili watu wahamasike wawe wanafanya hivyo, hizi shule ndo zitoazo Madiwani, Wabunge, Mawaziri, Maraisi, Masurveyor, Madaktari, Waandishi wa Habari, Waalimu, Mama Lishe, Kuli,Wakurugenzi,n.k
Waalimu wakiwa wame pose ofisini kwao. Samahani post ni ndefu sana, lakini nadhani mmeweza kuipata nia yangu, tupende tulikotoka, OLD IS GOLD |
duh inabidi namie niende kutembelea shule yangu this time ni kirudu home.
ReplyDeleteUfanye hivyo my dear, utuhadithie yaliyojiri huko na yanayoendelea
ReplyDeleteYaani nimeangalia picha hizi huku akili yangu ikiwa Nganza sekondari, nakumbuka tulivyokuwa tukifua, tukivusha vyakula kupeleka mabwenini, tulivyokuwa kukikimbia mchakamchaka..prepo kabla ya kulala na mengine meeengi, aiseee Esta umenipa wazo, nami Nganza nitarudi.
ReplyDeleteUbarikiwe sana.
Da Mija kumbe ulisoma Nganza? Nami nilisoma huko, siku nilipoenda wala sikuwa na Camera, nenda mamie ukaone jinsi siku hizi ni A Level tuuu, no O level tena
ReplyDeleteNijambo jema kukumbuka tulipotoka,Kazi nzuri.
ReplyDelete