Pages

Friday, February 24, 2012

GOOD MEMORIES @BAGAMOYO PRIMARY SCHOOL - TUKUYU

Michuzi Jr. anaelezea matembezi yake aliyofanya kwenye shule ya msingi aliyosoma
Nilimaliza hapa darasa la saba mwaka mnamo mwaka 1988
Hivi ndivyo shule ilivyokuwa ikionekana kwa mbele enzi hizo,na sehemu ya uwanja wa kuchezea michezo safi kabisa, hizo nyumba ndogo mbele (haaa haaa) ni Vyoo,vya Kike na Kiume
Ni mlango mkuu wa kuingilia waalimu tu kwenda kwenye ofisi zao kama zinavyoonekana,ukikatiza tu hapo ujue umeitwa na mwalimu vinginevyo haikuwa ruhusa kukatiza hapo
Bango la shule yenyewe
NIlikuwa nikitembea umbali wa kilometa 4 mpaka kufika shuleni.Mara ya mwisho kuitembelea shule hii ni mapema mwaka jana (2011) na kuikuta imechakaa kwa kiasi hiki,na kwa bahati mbaya sikumkuta hata mwalimu mmoja aliyenifundisha,wengine walihamishwa  na wengine walifariki (Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi-Amin)
Asante sana Michuzi Jr. kwa kushare nasi matembezi uliyoyafanya shule uliyosoma, ni kumbukumbu nzuri na inakukumbusha ulikotoka kwani kwa sasa kupitia mwanzo wa shule hiyo, na km ulizotembea kwa sasa unakula kuku kwa mrija

No comments:

Post a Comment